Ramani ya mkoa wa Manyara |
Hanang ni moja kati ya wilaya tano zilizopo katika
mkoa wa manyara nchini Tanzania. Ipo umbali wa kilomita 242 kusini magharibi
mwa Arusha, na km 197 kwa kipimo cha anga (Flight Distance). Kwa upande wa
kaskazini imepakana na wilaya ya Mbulu na Babati, kusini mashariki ni mkoa wa
Dodoma, na kusini magharibi ni mkoa wa Singida. Kulingana na sensa ya mwaka
2012 wilaya ya hanang ilikuwa na jumla ya watu 275,990.
Wilaya
ya hanang imegawanywa katika kata 25 ambazo ni:
· Balangdalalu
- Bassodesh
- Bassotu
- Dirma
- Endasak
- Endasiwold
- Ganana
- Gehandu
- Gendabi
- Getanuwas
- Gidahababieg
- Gisambalang
- Gitting
- Hidet
- Hirbadaw
- Katesh
- Lalaji
- Laghanga
- Masakta
- Masqaroda
- Measkron
- Mogitu
- Nangwa
- Simbay na
- Sirop
Watu na style za maisha
Ramani ya Wilaya ya Hanang |
Wilaya ya Hanang imekaliwa na makabila makubwa mawili ambayo ni Wairaqw na Wabarbaig. Wabarabaig wamekuwa kivutio kikubwa sana cha watalii wa nje kutokana na tamaduni zao ambazo hazijaathiriwa sana na tamaduni za kimagharibi. Wageni wamekuwa wakivutiwa sana na mavazi ya asili ya ngozi kwa wanawake na mashuka mekundu maarufu kama migorori iliyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kupambwa na shanga za rangi mbambali na vifungo vilivyoshonwa kwa ufundi na kuwekwa marinda maarufu kama “sapsapt”
Wageni wako huru kujichanganya na makabila
haya na kupokelewa kwa ukarimu kama ilivyo asili ya makabila haya.
Kama unapeda ndege Hanang ndo sehemu ya
kuwaona kwani kuna zaidi spishi 400 za ndege watakaokusindikiza kwa nyimbo
kipindi chote utakapokua unatembelea maeneo tofauti ya wilaya hii.
No comments:
Post a Comment