Katika kuhakikisha kuwa
ahadi zote za chama cha mapinduzi zinatekelezwa kama zilivyoahidiwa katika
ilani ya uchaguzi mwaka 2010, katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndg. Abrahaman
Kinana amezuru wilaya ya Hanang’ tarehe 27th May 2014, ikiwa ni siku
ya kwanza ya ziara yake ya siku saba mkoani Manyara. Katibu mkuu ameongozana katibu mwenezi
wa CCM kijana machachari Nape Nauye, Mbunge wa Hanang’ na waziri wa uwekezaji
na uwezeshwaji Mhe. Mary Nagu, Waziri mkuu wa zamani Mhe. Fredrick Sumaye na
makada wengine wa Chama cha Mapindzi.
Akihutubia katika
viwanja vya chama cha mapinduzi vilivyokuwa vimefurika watu hadi kukosa sehemu
ya kusimama Ndg. Kinana aliwataka wananchi wa wilaya ya Hanang kuacha kupiga
zogo za kisiasa na kufanya shughuli za maendeleo zitakazowaingizia kipato.
Akizungumza kwa
msisitizo Ndg. Kinana aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika
kuleta maendeleo kwa kutokataa kutoa michango muhimu akitolea mfano mchango wa
kujenga maabara katika shule za sekondari, na ujenzi wa hospitali, pia
aliwataka wafanyabiashara kukaa na madiwani wao kama wanaona kodi ni kubwa ili
wapunguziwe kwani madiwani wengi sio wafanyabiashara hivyo hawajui tamu na
chungu ya biashara.
Aidha kuhusu migogoro
ya ardhi ikiwemo Mashamba ya NAFCO ngd. Kinana aliahidi kuwa wawekezaji wote
wanaokodisha mashamba hayo watachukuliwa kama wameshindwa kuyaendeleza na
watanyang’anywa na kurudishwa kwa wananchi. Pia alisisitiza kuwa sio azma ya
serikal kumpa mwekezaji moja mkubwa ili yeye awakodishie watu wengine
kidogokidogo, mbunge wa wilaya Hanang’ alimuunga mkono kwa hilo kwa kusisitiza
kuwa wawekezaji wote wanaokodisha mashamba hayo watanyang’anywa na kurudishwa
kwa wananchi.
Na mwisho kuhusu katiba
mpya Ndg. Kinana alisema muundo wa serikali hauleti vyakula mezani mwetu wala
fedha mifukoni mwetu na kusisitiza kuwa CHADEMA wanataka serikali tatu kwa uchu
wa madaraka tu na sio kwa kuwatakia mema watanzania, Ndg. Kinana alisisitiza
kuwa chadema wanaamini kuwa zikiundwa serikali tatu, wao watashinda bara, CUF
watashinda Zanzibar na CCM watachukua serikali ya tatu ya shirikisho. Aidha
ndugu kinana alisema kuwa katika bunge la katiba tumeshuhudia kigeugeu cha
chadema wakitaka mara kura ya wazi, mara siri, na pia kwa kipindi chote
wamekuwa wakizungumzia mgawanyo wa madaraka badala ya kero za wananchi.
Akiendelea kutolea ufafanuzi ndg. Kinana alisema katiba ya Tanzania imefanyiwa
marekebisho mara 14 kwa kipindi cha miaka 50 tangu tupate uhuru, lakini katiba
ya marekani imefanyiwa marekebisho mara saba tu kwa muda wa zaidi ya miaka 280.
<swali> Je, katiba yetu ni bora kuliko ya marekani au ni kama nguo
iliyochakaa kwa kupigwa viraka kila sehemu?
Baada ya hotuba nzuri
ya Ngd. Kinana ailgawa mizinga 140 kwa vikundi kumi vya ujasiriamali na pia
kugawa kadi kwa wana wapotevu waliorudi kundini kwa kurudisha kadi za chadema
na kuchukua kadi zao mpya za CCM.
No comments:
Post a Comment