Monday, 17 March 2014

The Origin of Hanang Vijana SACCOS

Katika kuttekeleza sera ya Chama Cha Mapinduzi, Mkuu wa wilaya ya Hanang
Mh. Christina Mndeme, aliwakutanisha vijana kutoka kata zote za wilaya ya Hanang, na baada ya kujadili changamoto za kimaisha zinazowakabili vijana hao kwa pamoja walikubaliana kuanzisha SACCOS ambayo itakuwa chombo cha kuwaunganisha vijana hao na kutoa mikopo yenye masharti nafuu, itakayowawezesha vijana hao kujikomboa kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Christina Mndeme.


Akizungumza na gazeti hili mkuu wa wilaya ya Hanang alisema “Shirika hili lilianzishwa kwa lengo la kuwakwamua vijana kichumi na kupanua wigo wa ajira kwa vijana na kuamsha vipaji na uwezo wao wa kufanya kazi kwa kuunda vikundi vidogovidogo vya wajasiriamali na kuwapa elimu na mikopo yenye masharti nafuu itakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuwa chachu ya maendeleo yao, jamii inayowazunguka na Wilaya kwa ujumla”
Akitolea ufafanuzi mkuu wa wilaya ya Hanang alisema wameanzisha vikundi vitano ambavyo ni kikundi cha wafuga nyuki, waendesha bodaboda, kilimo, wafugaji wa kuku wa kienyeji na kikundi cha wafyatua matofali ya kisasa kwa technolojia ya hydroform,

Taskforce ya Hanang Vijana Saccos

Akaindelea kufafanua mkuu wa wilaya ya Hanang alisema “Shirika hili lilianzishwa chini ya sheria ya vyama vya ushirika na 20 ya mwaka 2003, na kanuni za vyama vya ushirika za mwaka 2004, na kusajiliwa tarehe 04/12/2013 kwa nambari ya usajili MNR/144 Ikiwa na wanachama waanzilishi 316, na sasa tunajivunia kuwa na wanachama hai zaidi ya 400 na bado tunawahamasisha wote wa kike na wa kiume waishio wilaya ya Hanang wenye umri kati ya miaka 15 na 35 wajiunge na Saccos hii”

Aidha mwenyekiti wa kamati ya mpito ya SACCOS hiyo Bw. Dominick Duncan alisema kuwa “Hii inaonesha nia ya dhati ya serikali katika kutokomeza umasikini, na kuwakomboa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa” akaongeza “Vijana wengi tulikuwa hatuna ajira rasmi, hivyo hatukuwa na kipato cha uhakika, hii ilitupelekea vijana wengi kukosa matumaini na kujiona kama kundi lililosahaulika katika jamii, lakini SACCOS hii imefufua matumaini yetu, na leo najivunia kuwa kijana wa kitanzania” 

Thursday, 27 February 2014

Tangazo

Ndugu wajumbe wa Hanang Vijana Saccos, tunasikitika kuwatangazia kuwa uzinduzi wa saccos yetu umeahirishwa mpaka hapo tutakapopewa taarifa rasmi. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Tuesday, 25 February 2014

TANGAZO

VIJANA WOTE WA WILAYA YA HANANG, MNAKARIBISHWA KWENYE UZINDUZI WA SACCOS YA VIJANA WA HANANG SIKU YA TAREHE 01/03/2014 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI KATESH, KUANZIA SAA TATU KAMILI ASUBUHI (9:00AM), MGENI RASMI ATAKUWA WAZIRI WA VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO Mhe. Dk. FENELLA MUKANGARA, WAZIRI WA UWEZESHWAJI NA UWEKEZAJI NA MBUNGE WA HANANG Mhe. Dk. MARY NAGU, NA PIA WAGENI WAALIKWA KUTOKA NATIONAL HOUSING CORPORATION (NHC), BARAZA LA UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI TANZANIA VIONGOZI WA WILAYA, MKOA NA VIONGOZI WENGINE WA KITAIFA.
VIJANA WOTE MNAKARIBISHWA KATIKA UZINDUZI HUO. 
 
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA:
M/KITI WA TASKFORCE: DOMINICK DUNCAN
AU WAFIKE OFISI YA VYAMA VYA USHIRIKA: KILIMO KATESH.
AU PIGA SIMU NO.
0766988891
0786230675

Wednesday, 19 February 2014

TANGAZO

Wajumbe wa HANANG VIJANA SACCOS, nasikitika kuwataarifu kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, Uchaguzi  umehairishwa mpaka hapo mtakapopewa taarifa zaidi. Samahani kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Monday, 17 February 2014

TANGAZO

Ndugu wanachama wa HANANG VIJANA SACCOS mnakaribishwa kwenye kikao cha uchaguzi utakaofanyika tarehe 20/02/2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang Saa Tatu kamili asubuhi(09:00AM) Kwa maelezo zaidi piga simu na:
                                                      0784 – 157386
0766 -  988891

Friday, 14 February 2014

Lengo Kuu

Hanang Vijana Saccos ina lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi na kuamsha vipaji na uwezo wao wa kufanya kazi kwa kuunda vikundi vidogovidogo vya wajasiriamali na kuwapa elimu na mikopo yenye masharti nafuu itakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuwa chachu ya maendeleo yao, jamii inayowazunguka na Wilaya kwa ujumla.

Integrity

We seek to do what is right and treat others with honesty, respect, and dignity. We make clear when we know something and when we believe something—and communicate both.