Thursday 27 February 2014

Tangazo

Ndugu wajumbe wa Hanang Vijana Saccos, tunasikitika kuwatangazia kuwa uzinduzi wa saccos yetu umeahirishwa mpaka hapo tutakapopewa taarifa rasmi. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Tuesday 25 February 2014

TANGAZO

VIJANA WOTE WA WILAYA YA HANANG, MNAKARIBISHWA KWENYE UZINDUZI WA SACCOS YA VIJANA WA HANANG SIKU YA TAREHE 01/03/2014 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI KATESH, KUANZIA SAA TATU KAMILI ASUBUHI (9:00AM), MGENI RASMI ATAKUWA WAZIRI WA VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO Mhe. Dk. FENELLA MUKANGARA, WAZIRI WA UWEZESHWAJI NA UWEKEZAJI NA MBUNGE WA HANANG Mhe. Dk. MARY NAGU, NA PIA WAGENI WAALIKWA KUTOKA NATIONAL HOUSING CORPORATION (NHC), BARAZA LA UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI TANZANIA VIONGOZI WA WILAYA, MKOA NA VIONGOZI WENGINE WA KITAIFA.
VIJANA WOTE MNAKARIBISHWA KATIKA UZINDUZI HUO. 
 
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA:
M/KITI WA TASKFORCE: DOMINICK DUNCAN
AU WAFIKE OFISI YA VYAMA VYA USHIRIKA: KILIMO KATESH.
AU PIGA SIMU NO.
0766988891
0786230675

Wednesday 19 February 2014

TANGAZO

Wajumbe wa HANANG VIJANA SACCOS, nasikitika kuwataarifu kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, Uchaguzi  umehairishwa mpaka hapo mtakapopewa taarifa zaidi. Samahani kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Monday 17 February 2014

TANGAZO

Ndugu wanachama wa HANANG VIJANA SACCOS mnakaribishwa kwenye kikao cha uchaguzi utakaofanyika tarehe 20/02/2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang Saa Tatu kamili asubuhi(09:00AM) Kwa maelezo zaidi piga simu na:
                                                      0784 – 157386
0766 -  988891

Friday 14 February 2014

Lengo Kuu

Hanang Vijana Saccos ina lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi na kuamsha vipaji na uwezo wao wa kufanya kazi kwa kuunda vikundi vidogovidogo vya wajasiriamali na kuwapa elimu na mikopo yenye masharti nafuu itakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuwa chachu ya maendeleo yao, jamii inayowazunguka na Wilaya kwa ujumla.

Integrity

We seek to do what is right and treat others with honesty, respect, and dignity. We make clear when we know something and when we believe something—and communicate both.

Tuesday 11 February 2014

About Us

Hanang Vijana Saccos ni shirika la kuweka na kukopa la vijana wanaoishi wilaya ya Hanang, lenye lengo la kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na kuunda vikundi vya wajasiriamali ili kuwajengea vijana hao uwezo wa kujiajiri.