Thursday 29 May 2014

KUHUSU HANANG


Ramani ya mkoa wa Manyara
Hanang ni moja kati ya wilaya tano zilizopo katika mkoa wa manyara nchini Tanzania. Ipo umbali wa kilomita 242 kusini magharibi mwa Arusha, na km 197 kwa kipimo cha anga (Flight Distance). Kwa upande wa kaskazini imepakana na wilaya ya Mbulu na Babati, kusini mashariki ni mkoa wa Dodoma, na kusini magharibi ni mkoa wa Singida. Kulingana na sensa ya mwaka 2012 wilaya ya hanang ilikuwa na jumla ya watu 275,990.

Wilaya ya hanang imegawanywa katika kata 25 ambazo ni:

·   Balangdalalu
  • Bassodesh
  • Bassotu
  • Dirma
  • Endasak
  • Endasiwold
  • Ganana
  • Gehandu
  • Gendabi
  • Getanuwas
  • Gidahababieg
  • Gisambalang
  • Gitting
  • Hidet
  • Hirbadaw
  • Katesh
  • Lalaji
  • Laghanga
  • Masakta
  • Masqaroda
  • Measkron
  • Mogitu
  • Nangwa
  • Simbay na
  • Sirop

Watu na style za maisha
Ramani ya Wilaya ya Hanang

Wilaya ya Hanang imekaliwa na makabila makubwa mawili ambayo ni Wairaqw na Wabarbaig. Wabarabaig wamekuwa kivutio kikubwa sana cha watalii wa nje kutokana na tamaduni zao ambazo hazijaathiriwa sana na tamaduni za kimagharibi. Wageni wamekuwa wakivutiwa sana na mavazi ya asili ya ngozi kwa wanawake na mashuka mekundu maarufu kama migorori iliyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kupambwa na shanga za rangi mbambali na vifungo vilivyoshonwa kwa ufundi na kuwekwa marinda maarufu kama “sapsapt”

Wageni wako huru kujichanganya na makabila haya na kupokelewa kwa ukarimu kama ilivyo asili ya makabila haya.


Kama unapeda ndege Hanang ndo sehemu ya kuwaona kwani kuna zaidi spishi 400 za ndege watakaokusindikiza kwa nyimbo kipindi chote utakapokua unatembelea maeneo tofauti ya wilaya hii. 

Wednesday 28 May 2014

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA NDUGU ABRAHAMAN KINANA KATIKA ZIARA YAKE WILAYANI HANANG’ TAREHE 27/5/2014.


Katika kuhakikisha kuwa ahadi zote za chama cha mapinduzi zinatekelezwa kama zilivyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi mwaka 2010, katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndg. Abrahaman Kinana amezuru wilaya ya Hanang’ tarehe 27th May 2014, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku saba mkoani Manyara. Katibu mkuu ameongozana katibu mwenezi wa CCM kijana machachari Nape Nauye, Mbunge wa Hanang’ na waziri wa uwekezaji na uwezeshwaji Mhe. Mary Nagu, Waziri mkuu wa zamani Mhe. Fredrick Sumaye na makada wengine wa Chama cha Mapindzi.

Akihutubia katika viwanja vya chama cha mapinduzi vilivyokuwa vimefurika watu hadi kukosa sehemu ya kusimama Ndg. Kinana aliwataka wananchi wa wilaya ya Hanang kuacha kupiga zogo za kisiasa na kufanya shughuli za maendeleo zitakazowaingizia kipato.

Akizungumza kwa msisitizo Ndg. Kinana aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika kuleta maendeleo kwa kutokataa kutoa michango muhimu akitolea mfano mchango wa kujenga maabara katika shule za sekondari, na ujenzi wa hospitali, pia aliwataka wafanyabiashara kukaa na madiwani wao kama wanaona kodi ni kubwa ili wapunguziwe kwani madiwani wengi sio wafanyabiashara hivyo hawajui tamu na chungu ya biashara.

Aidha kuhusu migogoro ya ardhi ikiwemo Mashamba ya NAFCO ngd. Kinana aliahidi kuwa wawekezaji wote wanaokodisha mashamba hayo watachukuliwa kama wameshindwa kuyaendeleza na watanyang’anywa na kurudishwa kwa wananchi. Pia alisisitiza kuwa sio azma ya serikal kumpa mwekezaji moja mkubwa ili yeye awakodishie watu wengine kidogokidogo, mbunge wa wilaya Hanang’ alimuunga mkono kwa hilo kwa kusisitiza kuwa wawekezaji wote wanaokodisha mashamba hayo watanyang’anywa na kurudishwa kwa wananchi.

Na mwisho kuhusu katiba mpya Ndg. Kinana alisema muundo wa serikali hauleti vyakula mezani mwetu wala fedha mifukoni mwetu na kusisitiza kuwa CHADEMA wanataka serikali tatu kwa uchu wa madaraka tu na sio kwa kuwatakia mema watanzania, Ndg. Kinana alisisitiza kuwa chadema wanaamini kuwa zikiundwa serikali tatu, wao watashinda bara, CUF watashinda Zanzibar na CCM watachukua serikali ya tatu ya shirikisho. Aidha ndugu kinana alisema kuwa katika bunge la katiba tumeshuhudia kigeugeu cha chadema wakitaka mara kura ya wazi, mara siri, na pia kwa kipindi chote wamekuwa wakizungumzia mgawanyo wa madaraka badala ya kero za wananchi. Akiendelea kutolea ufafanuzi ndg. Kinana alisema katiba ya Tanzania imefanyiwa marekebisho mara 14 kwa kipindi cha miaka 50 tangu tupate uhuru, lakini katiba ya marekani imefanyiwa marekebisho mara saba tu kwa muda wa zaidi ya miaka 280. <swali> Je, katiba yetu ni bora kuliko ya marekani au ni kama nguo iliyochakaa kwa kupigwa viraka kila sehemu?

Baada ya hotuba nzuri ya Ngd. Kinana ailgawa mizinga 140 kwa vikundi kumi vya ujasiriamali na pia kugawa kadi kwa wana wapotevu waliorudi kundini kwa kurudisha kadi za chadema na kuchukua kadi zao mpya za CCM.