Monday 17 March 2014

The Origin of Hanang Vijana SACCOS

Katika kuttekeleza sera ya Chama Cha Mapinduzi, Mkuu wa wilaya ya Hanang
Mh. Christina Mndeme, aliwakutanisha vijana kutoka kata zote za wilaya ya Hanang, na baada ya kujadili changamoto za kimaisha zinazowakabili vijana hao kwa pamoja walikubaliana kuanzisha SACCOS ambayo itakuwa chombo cha kuwaunganisha vijana hao na kutoa mikopo yenye masharti nafuu, itakayowawezesha vijana hao kujikomboa kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Christina Mndeme.


Akizungumza na gazeti hili mkuu wa wilaya ya Hanang alisema Shirika hili lilianzishwa kwa lengo la kuwakwamua vijana kichumi na kupanua wigo wa ajira kwa vijana na kuamsha vipaji na uwezo wao wa kufanya kazi kwa kuunda vikundi vidogovidogo vya wajasiriamali na kuwapa elimu na mikopo yenye masharti nafuu itakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuwa chachu ya maendeleo yao, jamii inayowazunguka na Wilaya kwa ujumla
Akitolea ufafanuzi mkuu wa wilaya ya Hanang alisema wameanzisha vikundi vitano ambavyo ni kikundi cha wafuga nyuki, waendesha bodaboda, kilimo, wafugaji wa kuku wa kienyeji na kikundi cha wafyatua matofali ya kisasa kwa technolojia ya hydroform,

Taskforce ya Hanang Vijana Saccos

Akaindelea kufafanua mkuu wa wilaya ya Hanang alisema “Shirika hili lilianzishwa chini ya sheria ya vyama vya ushirika na 20 ya mwaka 2003, na kanuni za vyama vya ushirika za mwaka 2004, na kusajiliwa tarehe 04/12/2013 kwa nambari ya usajili MNR/144 Ikiwa na wanachama waanzilishi 316, na sasa tunajivunia kuwa na wanachama hai zaidi ya 400 na bado tunawahamasisha wote wa kike na wa kiume waishio wilaya ya Hanang wenye umri kati ya miaka 15 na 35 wajiunge na Saccos hii”

Aidha mwenyekiti wa kamati ya mpito ya SACCOS hiyo Bw. Dominick Duncan alisema kuwa “Hii inaonesha nia ya dhati ya serikali katika kutokomeza umasikini, na kuwakomboa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa” akaongeza “Vijana wengi tulikuwa hatuna ajira rasmi, hivyo hatukuwa na kipato cha uhakika, hii ilitupelekea vijana wengi kukosa matumaini na kujiona kama kundi lililosahaulika katika jamii, lakini SACCOS hii imefufua matumaini yetu, na leo najivunia kuwa kijana wa kitanzania” 

No comments:

Post a Comment